Synopsis.

Kisa ni kati ya vijana wanne wanaotengana na kusababishiana mauti kwa sababu ya tamaa ya mmoja wao.
Riziki pale chumbani alipokuwa amelala kando ya Hasira aliona uhusiano wao kama nyavu zilizoshikana kukandamiza maisha yake. Chumba hicho kilikuwa kimepakwa rangi ya hudhurungi kutani na katikati kukawa na bahari ya kitanda kilichokuwa na gondoro nyeupe na suka za rangi ya dhahabu.